Balagha Katika Hotuba za Wagombea Wawili wa Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022
Loading...
Date
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Embu
Abstract
Balagha ni mkakati ambao hutumika katika mawasiliano ili kushawishi
hadhira lengwa. Utafiti huu ulilenga kuchanganua matumizi ya balagha
katika hotuba za wagombea wawili wa urais, wakati wa makongamano yao
ya kitaifa ya wajumbe nchini Kenya, mwaka wa 2022. Wagombea hao
walikuwa William Samoei Ruto na Raila Odinga. Utafiti uliongozwa na
nadharia ya Balagha ya Aristotle. Nadharia hii, ilisaidia mtafiti katika
kutambua matumizi ya balagha, maadili, kigusahisi na mantiki kama
yalivyothibitika katika hotuba nne zilizowasilishwa. Data ya utafiti huu
ilikusanywa kutoka kwa rekodi rasmi za hotuba hizo kutoka kwa mtandao
wa YouTube. Mtafiti alitumia mbinu ya kimakusudi kuangazia matumizi ya
balagha katika hotuba zilizotolewa na wagombea wawili wakuu wa urais. Hii
ni kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu katika siasa na nafasi yao ya
kipekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Data ilichanganuliwa kwa
njia ya kimaelezo kwa kufuata mihimili ya nadharia ya balagha. Matokeo ya
utafiti huu yalidhihirisha matumizi ya aina tatu kuu za balagha ambazo ni;
mantiki, kigusahisi na maadili. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa
kujenga imani, kugusa hisia, kuonyesha uwezo wa uongozi, na kueleza sera
zao. Kazi hii inatarajiwa kuwa na mchango muhimu kwa usomi katika
uwanja wa lugha na mawasiliano, mawasiliano ya kisiasa na kusaidia
wanajamii kupata maarifa ya kuwawezesha kung’amua ghiliba za
wagombea. Utafiti ulihitimisha kuwa balagha ina jukumu muhimu katika
mawasiliano ya kisiasa na ushawishi wa wapiga kura. Hata hivyo, balagha
inafaa itumike kwa ujuzi na si kwa lengo la kuidanganya hadhira lengwa bali
kwa kutumia urazini na maadili katika azma ya wagombea.
Description
Keywords
Citation
Kamuru, C., Wanyama, J., & M’Ngaruthi, T. (2025). Balagha Katika Hotuba za Wagombea Wawili wa Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022. East African Journal of Swahili Studies, 8(1), 490-504. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.3230