Umbuji wa Wahusika katika Ushairi wa Kiswahili: Mifano Kutoka kwa Diwani ya Jicho la Ndani (S.A. Mohamed, 2002).

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Suala la utunzi na uhakiki wa mashairi ya Kiswahili limejadiliwa kwa muda mrefu na washairi na wataalamu mbalimbali. Mjadala huu umejikita katika dhana na maana ya shairi la Kiswahili na iwapo lihakikiwe kwa kuzingatia kaida zilizowekwa na wanamapokeo au uhuru ulioibuliwa na wanamapinduzi. Hali hii imekinza kwa kiasi fulani uzingatiaji kikamilifu wa mbinu nyinginezo za kiubunifu za kulihakiki shairi la Kiswahili. Kati ya vipengele muhimu katika sanaa hii kongwe vilivyotelekezwa kiasi ni uteuzi wa wahusika, uchunguzi wa mazingira wanamopatikana na hisia wanazotumiwa na mshairi kuwasilisha, kama inavyosisitizwa katika Nadharia ya Ulimbwende. Kimsingi, jamii husawiriwa katika kazi za fasihi kupitia wahusika kwani ndio wawakilishi na viwakilishi vya hali halisi za wanajamii. Jinsi mshairi akatavyowateua na kuwasawiri wahusika wake katika mazingira mahsusi itaifanya hadhira kuyapenda au kuyachukia matendo, tabia na hali fulani za wanajamii waliowakilishwa na wahusika hao. Makala haya yananuiwa kubainisha dhima ya wahusika wa kishairi katika kujadili na kuhifadhi masuala ya kihistoria.
Description
Keywords
Ushairi wa Kiswahili, usawiri wa wahusika, wahusika wa kishairi, historia
Citation
East African Scholars Journal of Education, Humanities and Literature Volume-2, Issue-6,| Jun-2019