Articles: Department of Humanities
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Articles: Department of Humanities by Subject "balagha"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Ubandikaji Majina na Majumlishi Memeto kama Mikakati ya Propaganda Katika Mdahalo wa Urais wa Kenya 2013(2018-12) Wanyama, John K.; Wandera, P. SimwaWanasiasa hutumia mbinu anuai kuelekeza uelewa wa suala la kisiasa; mikakati ya propaganda haswa ndiyo hutumika zaidi katika kampeni za kisiasa miongoni mwa wanadamu wote ulimwenguni. Shida kubwa ni kama jamii ya kistarabu na kibinadamu inaweza kuendelea kuthamini na kushiriki katika propaganda katika shughuli za uteuzi wa uongozi: kwani kwenye propaganda huwa kupiga chuku,uongo, chuki na mambo mengi ambayo ni kinyume na kutangamana kwa wanadamu kama washiriki wenza katika jamii. Kazi hii imetathmini namna mikakati miwili ilitumiwa na wagombea wa kiti cha urais nchini Kenya, mwaka wa 2013, kwa lengo la kushawishi wapiga kura na kujipa umaarufu. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Matini. Data ilikuwa kauli zilizoingiana na mikakati ya propaganda. Uchanganuzi ulizingatia maarifa ya kithamani, ya kimaudhui na kiuhakiki. Matokeo yalionyesha matumizi ya ubandikaji majina na majumlishi memeto. Tekniki hizi zilitumiwa na wagombea kwa lengo la kujijengea sifa njema huku wakilenga kubomoa sifa za wapinzani. Pia zilitumiwa kwa dhamira ya kuuza sera za vyama vyao huku wakidhamiria kudhalilisha sera za wapinzani. Kazi hii ni mchango adimu kwa taaluma ya uchanganuzi matini na mawasiliano ya kisiasa. Aidha ni ya manufaa kwa wanafunzi wa uchanganuzi matini, sayansi ya siasa na mawasiliano. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kuhusu mbinu nyingine kama vile balagha, na pia kuzingatia nadharia zingine tofauti zinazohusu uchanganuzi wa matini.