Browsing by Author "Mwembu, Kimathi"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia(2022) Mwembu, Kimathi; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia..Item Uhusiano wa Kifahiwa katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Leksika Pragmatiki(2022) Mwembu, Kimathi; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.Makala haya yanalenga kubainisha jinsi fahiwa zinavyohusiana katika leksia za Kîîtharaka kwa kuzingatia mtazamo wa leksika pragmatiki.Ubadili maana katika leksia mbalimbali husababisha kutokea uhusiano wa kifahiwa katika leksia moja, na kati ya leksia mbili au zaidi. Katika makala haya, ubadili maana unaozua uhusiano wa kifahiwa katika leksia za Kîîtharaka umeangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Matokeo yanabainisha kwamba ubadili maana ukitokea katika leksia za Kîîtharaka, mahusiano ya kifahiwa yafuatayo hutokea: uhusiano wa kipolisemia, kihomnimia, kisinonimia, kihaiponimia, kimeronimu na kiantonimu. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na uhusiano na maana nyingine ya leksia iyo hiyo au leksia nyingine tofauti. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha ya leksia.