Repository logo
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
Repository logo
  • Communities & Collections
  • All of DSpace
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Mugambi, Allan"

Now showing 1 - 4 of 4
Results Per Page
Sort Options
  • No Thumbnail Available
    Item
    Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia
    (2022) Mwembu, Kimathi; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.
    Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia..
  • No Thumbnail Available
    Item
    Ubainishaji wa vigezo vya Utoaji Wa Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya
    (2022) Mutegi, David Micheni; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.
    Utafiti huu wa kionomastiki ulilenga kuchanganua vigezo vya utoaji wa toponemia za shule za msingi katika jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na Muthambi, jimboni dogo la Maara kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi, nchini Kenya. Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini ziliongoza utafiti huu. Data ilikusanywa kupitia mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu walikuwa wenyeji wa eneo la utafiti na iliaminika kuwa wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka 70 na zaidi ilichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa kuwa walikuwa wakipokea marupurupu maalum kutoka kwa serikali, na hivyo walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia hutolewa kwa kuzingatia vigezo vya kimaumbile, kiuchumi na kijamii. Matokeo ya utafiti huu yatatoa marejeleo muhimu kwa watafiti wa baadaye watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi na lugha nyinginezo.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Uhusiano wa Kifahiwa katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Leksika Pragmatiki
    (2022) Mwembu, Kimathi; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.
    Makala haya yanalenga kubainisha jinsi fahiwa zinavyohusiana katika leksia za Kîîtharaka kwa kuzingatia mtazamo wa leksika pragmatiki.Ubadili maana katika leksia mbalimbali husababisha kutokea uhusiano wa kifahiwa katika leksia moja, na kati ya leksia mbili au zaidi. Katika makala haya, ubadili maana unaozua uhusiano wa kifahiwa katika leksia za Kîîtharaka umeangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Matokeo yanabainisha kwamba ubadili maana ukitokea katika leksia za Kîîtharaka, mahusiano ya kifahiwa yafuatayo hutokea: uhusiano wa kipolisemia, kihomnimia, kisinonimia, kihaiponimia, kimeronimu na kiantonimu. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na uhusiano na maana nyingine ya leksia iyo hiyo au leksia nyingine tofauti. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha ya leksia.
  • No Thumbnail Available
    Item
    Upambanuzi wa Miundo ya Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya
    (2022) Mutegi, David Micheni; Mugambi, Allan; Kinoti, Timothy M.
    Makala hii imewasilisha uchunguzi uliofanywa kuhusu michakato na mbinu zilizotumika katika uundaji wa toponemia katika jamii. Lengo mahsusi la utafiti huu lilikuwa kupambanua miundo ya toponemia katika eneo la Mwimbi na Muthambi jimboni dogo la Maara. Maeneo haya yaliteuliwa kwa vile yalihusiana kilugha na kiutamaduni hasa katika suala la onomastiki. Nadharia ya Ujinaishaji ndiyo ilitumiwa kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kupitia kwa ya mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala, na hivyo wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee iliweza kupatikana kwa urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha michakato mbalimbali ya uundaji wa toponemia katika jamii.

University of Embu | Library Website | MyLOFT | Chat with Us

© University of Embu Digital Repository. All Rights Reserved.