Uchanganuzi wa Mtindo Katika Muziki wa Benga wa Jamii ya Wakamba Mkabala wa Umtindo
| dc.contributor.author | Carolyne Muthini Mutuku | |
| dc.date.accessioned | 2025-12-02T12:57:43Z | |
| dc.date.available | 2025-12-02T12:57:43Z | |
| dc.date.issued | 2025-10-01 | |
| dc.description.abstract | Muziki ni njia mojawapo ambayo watu katika jamii hutumia kuwasilisha masuala kama vile mapenzi, kifo na siasa. Utafiti huu ulichanganua jinsi waimbaji wa muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba hutumia vipengele vya mtindo kuwasilisha jumbe. Kwa kuzingatia kielelezo cha nadharia ya umtindo ya Geoffrey Neil Leech, utafiti huu ulichunguza viwango vitatu vya mtindo ambavyo ni udhihirikaji, umbo na semantiki. Nadharia ya umtindo hufasiri na kuhakiki tungo kwa kuzingatia mtazamo wa kiisimu kama taaluma iliyo na uhusiano wa karibu na fasihi. Utafiti ulilenga: kubainisha mikakati ya kimtindo wanayotumia waimbaji wa muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba kuwasilisha ujumbe; kuchanganua wanavyoimarisha ujumi katika muziki wao; kueleza athari lengwa ya uchaguzi wao wa kimtindo. Ukusanyaji wa data ulitegemea mbinu ya uchanganuzi matini ili kuwezesha uchunguzi wa kina wa nyimbo za muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba zilizoteuliwa kimakusudi. Data ilichanganuliwa kimaelezo kwa kurejelea mihimili ya nadharia ya umtindo. Kutokana na utafiti huu ilibainika kuwa Waimbaji wa muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba hutumia vipengele vya kimtindo kama vile uradidi, urudiaji na tamathali za usemi kuwasilisha ujumbe. Vilevile utafiti uliweza kubaini kuwa waimbaji hao hutumia vipengele vya kimtindo kuimarisha ujumi wa kihalisia, kigothiki, kimapenzi, kisiasa na kitamaduni. Isitoshe, mikakati hii huwasaidia kufanikisha athari lengwa kwa hadhira zao. Utafiti huu unachangia maarifa mapya katika taaluma ya umtindo kwa kuonyesha jinsi vipengele vya kipekee vya lugha na usanii katika muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba vinavyojenga maana, kuhifadhi lugha za asili na kuakisi utambulisho wa kitamaduni. Unaimarisha vitengo vya isimu, fasihi na masomo ya tamaduni za Kiafrika. Pia, unatambulisha muziki wa Benga wa jamii ya Wakamba kama mada yenye umuhimu katika utafiti wa fasihi na lugha, huku ukiwaongoza wanamuziki kutunga muziki unaoangazia masuala ya kijamii na ujumi wa kisanaa | |
| dc.identifier.uri | http://repository.embuni.ac.ke/handle/123456789/4507 | |
| dc.language.iso | other | |
| dc.publisher | UoEm | |
| dc.title | Uchanganuzi wa Mtindo Katika Muziki wa Benga wa Jamii ya Wakamba Mkabala wa Umtindo |