Balagha Katika Hotuba za Wagombea Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022

dc.contributor.authorCaroline Kathure Kamuru
dc.date.accessioned2025-12-01T18:05:08Z
dc.date.available2025-12-01T18:05:08Z
dc.date.issued2025-10-01
dc.description.abstractBalagha ni mkakati unaotumiwa katika mawasiliano ili kushawishi hadhira lengwa. Utafiti huu ulilenga kuchanganua matumizi ya balagha katika hotuba za wagombea wawili wa kiti cha urais, wakati wa makongamano yao ya kitaifa ya wajumbe nchini Kenya, mwaka wa 2022. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kutathmini matumizi ya balagha katika hotuba za wagombea urais kwenye makongamano yao ya wajumbe nchini Kenya, 2022. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili. Nadharia ya balagha ya Aristotle iliongoza uchunguzi wa matumizi ya maadili, kigusahisi na mantiki kama zinavyothibitika katika hotuba zile. Nadharia ya vitendoneni ya Austin iliangazia vitendo dhamiriwa katika hotuba hizo nne. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka kwa rekodi rasmi za hotuba hizo kutoka kwa mtandao wa YouTube. Mtafiti alitumia mbinu ya kimakusudi kuteua hotuba zilizodhihirisha matumizi ya balagha na vitendo dhamiriwa katika hotuba za wagombea wawili wakuu wa urais. Hii ni kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu katika siasa na nafasi yao ya kipekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Mtafiti aliyateua makongamano haya kwani humpa mgombea nafasi nzuri ya kuwasilisha sera za chama na pia kuomba uungwaji mkono. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kufuata vigezo vya nadharia ya balagha ya Aristotle na nadharia ya vitendoneni ya Austin. Uwasilishaji wa matokeo ulifanywa kwa njia ya kimaelezo na jedwali. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa wagombea walitumia aina tatu kuu za balagha: mantiki, kigusahisi, na maadili ili kushawishi hadhira yao. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa kujenga imani, kugusa hisia, kuumua mihemko miongoni mwa wasikilizaji, kudhihirisha mantiki, kujenga imani mbele ya hadhira, kudhihirisha tajriba katika utekelezaji wa majukumu, kujinasibisha na hadhira, kuelekeza mtazamo wa hadhira na kushinda uchaguzi. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa kujenga imani ya wagombea, kugusa hisia na kueleza sera zao. Uchanganuzi wa vitendo dhamiriwa ulionyesha kuwa hotuba zilihusisha vitendo vya uwakilishaji, uelekezaji, uwajibikaji, uelezaji na matamko yaliyolenga kuathiri tabia ya wapiga kura. Utafiti ulihitimisha kuwa balagha ina jukumu muhimu katika mawasiliano ya kisiasa na ushawishi wa hadhira lengwa. Watafiti katika uwanja wa sayansi ya siasa, lugha na mawasiliano watapata maarifa muhimu kutoka kwa kazi hii yatakayochangia masomo yao na kazi ya utafiti katika viwango tofauti. Utafiti huu unapendekeza tafiti za baadaye ziangazie: Ulinganishaji wa mikakati ya balagha inavyotumika na wahusika malimbali wa kisiasa katika miktadha tofauti za kisiasa na kitamaduni na uchunguzi wa jinsi vyombo vya habari vya kijamii vinavyoshawishi ufanisi wa mikakati ya balagha. Utafiti huu unachangia katika kukuza mbinu bora za uongozi zinazohitajika kwa maendeleo endelevu nchini Kenya (SDG 16). Kinadharia, matokeo haya yanakuza uelewa kuhusu mbinu za mawasiliano katika muktadha wa kisiasa na jinsi zinavyotumika katika kuishawishi hadhira.
dc.identifier.urihttp://repository.embuni.ac.ke/handle/123456789/4504
dc.language.isoother
dc.publisherUoEm
dc.titleBalagha Katika Hotuba za Wagombea Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022
dc.typeThesis

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Balagha Katika Hotuba za Wagombea Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022.pdf
Size:
1.06 MB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: