Show simple item record

dc.contributor.authorKinoti, Timothy M.
dc.date.accessioned2020-08-14T12:07:07Z
dc.date.available2020-08-14T12:07:07Z
dc.date.issued2015-04
dc.identifier.urihttp://repository.embuni.ac.ke/handle/embuni/3402
dc.description.abstractUtafiti huu ulishughulikia usawiri wa mwanasiasa wa Afrika katika ushairi wa Kiswahili. Kimsingi, mtafiti alichunguza jinsi washairi mbalimbali walivyowasawiri wanasiasa wa Afrika kiubunifu kwa lengo la kudhihirisha walivyobadilika kisiasa na kimaadili kutoka enzi za ukoloni hadi kipindi cha siasa za vyama vingi. Utafiti huu ulichukulia kuwa wanasiasa hawa hutekeleza wajibu mkubwa katika maendeleo ya mataifa yao na bara la Afrika kwa jumla. Uafikiaji wa malengo mbalimbali ya maendeleo kama vile Ruwaza ya 2030 nchini Kenya na uimarishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa utategemea maamuzi ya kisiasa. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza nafasi ya ushairi wa Kiswahili katika uhifadhi wa historia ya mwanasiasa wa Afrika; kubainisha sifa za mwanasiasa wa Afrika kabla ya uhuru na kutathmini mabadiliko ya mwanasiasa wa Afrika baada ya uhuru kwa mujibu wa washairi wa Kiswahili. Mtafiti aliichukulia sauti ya mshairi kuwa sauti ya mwananchi ambaye ndiye huathiriwa na maamuzi na vitendo vya wanasiasa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ulimbwende iliyoasisiwa na William Wordsworth na Samuel Taylor Coleridge na Nadharia ya Baada-Ukoloni ambayo inahusishwa na kazi za Edward W. Said, Gayatri Chakravorty Spivak na Homi K. Bhabha. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambapo mbinu ya sampuli ya kudhamiria ilitumiwa kuteua data kutoka kwa diwani teule. Uchanganuzi wa kimaelezo ulizingatiwa ambapo mashairi yaliyoteuliwa yalihakikiwa kwa mujibu wa madhumuni ya utafiti. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza imejumuisha utangulizi. Katika sura ya pili pana mwauo wa maandishi yanayohusiana na utafiti huu pamoja na misingi ya kinadharia. Sura ya tatu imeshughulikia mbinu za utafiti zilizotumiwa katika utafiti huu. Katika sura ya nne na tano, data imechanganuliwa, kuwasilishwa na matokeo kujadiliwa. Hatimaye, sura ya sita inatoa mahitimisho na mapendekezo kutokana na utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa ushairi wa Kiswahili ni utanzu wa fasihi ulio na umuhimu mkubwa katika kuhifadhi matukio mbalimbali ya kihistoria. Kupitia uhifadhi huu, sifa na vitendo vya mwanasiasa wa Afrika vimebainika katika vipindi mbalimbali vya kisiasa. Imebainika kuwa mwanasiasa wa Afrika aliyeonekana kuwa mzalendo kabla ya uhuru alibadilika ghafla uhuru ulipopatikana na kuwa mkandamizaji wa umma alioapa kulinda. Aidha, wanasiasa walioonekana kutetea upatikanaji wa demokrasia ya vyama vingi hawajatekeleza demokrasia hiyo. Licha ya dosari zilizobainishwa na utafiti huu, ni dhahiri kuwa bara la Afrika bado lina wanasiasa wachache vielelezo ambao wanaweza kuigwa na wanasiasa wa wakati huu na wale wa baadaye. Matokeo ya utafiti huu yatawanufaisha wasomi wa Kiswahili, waandishi na washikadau wote wa masuala ya kisiasa barani Afrika na kwingineko ulimwenguni.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherChuka Universityen_US
dc.titleUsawiri wa Mwanasiasa wa Afrika Katika Ushairi wa Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record