Unyanyasikaji wa Wanaume katika Diwani za Tumbo Lisiloshiba na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine
Loading...
Date
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Embu
Abstract
Fasihi kama kioo cha jamii hutumia lugha kwa ufanifu mkubwa kutuchorea taswira kamili ya yale yanayotendeka katika jamii. Fasihi haizuki katika ombwe tupu. Hivyo basi utafiti huu ulichunguza unyanyasikaji wa wanaume katika jamii. Ulichunguza suala mtambuko ambalo linaathiri haki za wanaume kama inavyosawiriwa katika Diwani ya Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Alifa Chokocho na Dumu Kayanda na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine iliyohaririwa na Ken Walibora. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna wanaume hunyanyasika katika diwani teule. Ilikuafikia lengo hili, nadharia ya Mtagusano wa Vitambulisho ilitumiwa. Ni mojawapo ya nadharia za kijinsia. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba. Data ya utafiti ilikusanywa kwa kusoma hadithi teule kutoka diwani za Kiswahili zilizoteuliwa vitabu, majarida na makala mengine kutoka mitandaoni. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimaksudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kimaelezo kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini ikiongozwa na madhumuni ya utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo ya makala yalionyesha kuwa mwanamume hunyanyasika kwa namna nyingi kama vile: kula uroda nje ya ndoa, utengano wa kijamaa, kukataliwa uchumba, upyaro, kunyimwa chakula na kuchapwa. Vipengele vya utambulisho vinavyoshirikiana na kusababisha unyanyasikaji wa wanaume ni: uchumi, jinsia, tabaka, matarajio ya kijamii. Kipengele kinachosababisha unyanyasikaji wa wanaume zaidi ni kipengele cha uchumi. Uchunguzi huu utawafaa wasomi, wanajamii, na waandishi kwani watapata uelewa zaidi wa aina za unyanyasikaji unaotendewa wanaume na kutafuta mbinu za kuwaokoa kutoka kwa udhalimu huu. Vile vile utakuwa na mchango katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili.
Description
Keywords
Citation
Waithaka, E., Wanyama, J., & M’ngaruthi, T. (2025). Unyanyasikaji wa Wanaume katika Diwani za Tumbo Lisiloshiba na Maskini Milionea na Hadithi Nyingine. East African Journal of Swahili Studies, 8(2), 37-52. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3257