Ubainishaji wa vigezo vya Utoaji Wa Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya
View/ Open
Date
2022Author
Mutegi, David Micheni
Mugambi, Allan
Kinoti, Timothy M.
Metadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu wa kionomastiki ulilenga kuchanganua vigezo vya utoaji wa
toponemia za shule za msingi katika jamii. Utafiti ulifanyika katika eneo la Mwimbi na
Muthambi, jimboni dogo la Maara kwenye Kaunti ya Tharaka-Nithi, nchini Kenya.
Nadharia ya Ujinaishaji pamoja na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi na Matini
ziliongoza utafiti huu. Data ilikusanywa kupitia mahojiano ya ana kwa ana pamoja na
hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja
kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika
maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa
wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha
machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata
ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu walikuwa wenyeji wa
eneo la utafiti na iliaminika kuwa wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti.
Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka 70 na zaidi ilichaguliwa
kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya
uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli
ya wazee ilipatikana kwa urahisi kwa kuwa walikuwa wakipokea marupurupu maalum
kutoka kwa serikali, na hivyo walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji
wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali
la utafiti. Utafiti huu ulibainisha kuwa toponemia hutolewa kwa kuzingatia vigezo vya
kimaumbile, kiuchumi na kijamii. Matokeo ya utafiti huu yatatoa marejeleo muhimu kwa
watafiti wa baadaye watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya
Kimwimbi na Muthambi na lugha nyinginezo.