Uhusiano wa Kifahiwa katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Leksika Pragmatiki
View/ Open
Date
2022Author
Mwembu, Kimathi
Mugambi, Allan
Kinoti, Timothy M.
Metadata
Show full item recordAbstract
Makala haya yanalenga kubainisha jinsi fahiwa zinavyohusiana katika leksia
za Kîîtharaka kwa kuzingatia mtazamo wa leksika pragmatiki.Ubadili maana
katika leksia mbalimbali husababisha kutokea uhusiano wa kifahiwa katika
leksia moja, na kati ya leksia mbili au zaidi. Katika makala haya, ubadili maana
unaozua uhusiano wa kifahiwa katika leksia za Kîîtharaka umeangaziwa. Data
ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa
kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Matokeo yanabainisha kwamba
ubadili maana ukitokea katika leksia za Kîîtharaka, mahusiano ya kifahiwa
yafuatayo hutokea: uhusiano wa kipolisemia, kihomnimia, kisinonimia,
kihaiponimia, kimeronimu na kiantonimu. Makala haya yanahitimisha
kwamba, maana ya leksia huwa na uhusiano na maana nyingine ya leksia iyo
hiyo au leksia nyingine tofauti. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana
kimatumizi na maana kimuktadha ya leksia.