Mchango wa Lugha za Kiasili katika Uafikiaji wa Maendeleo Endelevu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2021-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Makala hii inajadili dhima ya lugha za kiasili, ikiwemo ya Kiswahili, katika kuafikia maendeleo endelevu barani Afrika. Kimsingi, asilimia kubwa ya wenyeji wa bara hili huishi katika maeneo ya mashambani na huzitumia lugha za kiasili katika mawasiliano ya kila siku. Kati ya sekta muhimu zinazoathiriwa na matumizi ya lugha ni pamoja na elimu, habari na mawasiliano, burudani, dini, uandishi na uchapishaji, utunzaji na uhifadhi wa mazingira, afya, kilimo na biashara. Aidha, upatikanaji wa maendeleo endelevu utategemea kwa kiasi kikubwa iwapo wananchi watashirikishwa katika aina mbalimbali za utafiti na matokeo yake kuwasilishwa kwa lugha wanayoielewa ili waweze kuyatekeleza. Makala hii inachukulia kuwa lugha inayo dhima kuu katika utekelezaji wa huduma na shughuli mbalimbali za kitaaluma.
Description
Keywords
lugha za kiasili, maendeleo endelevu, mawasiliano
Citation
East African Scholars Journal of Education, Humanities and Literature Volume-4 Issue-6