Kamuru Caroline KathureWanyama John Khaisie , PhDM’Ngaruthi Timothy Kinoti , PhD2026-02-152026-02-152025-06-30Kamuru, C., Wanyama, J., & M’Ngaruthi, T. (2025). Balagha Katika Hotuba za Wagombea Wawili wa Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022. East African Journal of Swahili Studies, 8(1), 490-504. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.32302707-3467http://repository.embuni.ac.ke/handle/123456789/4566Balagha ni mkakati ambao hutumika katika mawasiliano ili kushawishi hadhira lengwa. Utafiti huu ulilenga kuchanganua matumizi ya balagha katika hotuba za wagombea wawili wa urais, wakati wa makongamano yao ya kitaifa ya wajumbe nchini Kenya, mwaka wa 2022. Wagombea hao walikuwa William Samoei Ruto na Raila Odinga. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Balagha ya Aristotle. Nadharia hii, ilisaidia mtafiti katika kutambua matumizi ya balagha, maadili, kigusahisi na mantiki kama yalivyothibitika katika hotuba nne zilizowasilishwa. Data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka kwa rekodi rasmi za hotuba hizo kutoka kwa mtandao wa YouTube. Mtafiti alitumia mbinu ya kimakusudi kuangazia matumizi ya balagha katika hotuba zilizotolewa na wagombea wawili wakuu wa urais. Hii ni kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu katika siasa na nafasi yao ya kipekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kufuata mihimili ya nadharia ya balagha. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha matumizi ya aina tatu kuu za balagha ambazo ni; mantiki, kigusahisi na maadili. Utafiti uligundua kuwa balagha ilitumika hasa kujenga imani, kugusa hisia, kuonyesha uwezo wa uongozi, na kueleza sera zao. Kazi hii inatarajiwa kuwa na mchango muhimu kwa usomi katika uwanja wa lugha na mawasiliano, mawasiliano ya kisiasa na kusaidia wanajamii kupata maarifa ya kuwawezesha kung’amua ghiliba za wagombea. Utafiti ulihitimisha kuwa balagha ina jukumu muhimu katika mawasiliano ya kisiasa na ushawishi wa wapiga kura. Hata hivyo, balagha inafaa itumike kwa ujuzi na si kwa lengo la kuidanganya hadhira lengwa bali kwa kutumia urazini na maadili katika azma ya wagombea.otherBalagha Katika Hotuba za Wagombea Wawili wa Urais Kwenye Makongamano ya Wajumbe Nchini Kenya, Mwaka wa 2022Article