Show simple item record

dc.contributor.authorMutegi, David Micheni
dc.contributor.authorMugambi, Allan
dc.contributor.authorKinoti, Timothy M.
dc.date.accessioned2022-10-26T12:57:58Z
dc.date.available2022-10-26T12:57:58Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.citationEast African Scholars Journal of Education, Humanities and Literatureen_US
dc.identifier.urihttp://repository.embuni.ac.ke/handle/123456789/4156
dc.description.abstractMakala hii imewasilisha uchunguzi uliofanywa kuhusu michakato na mbinu zilizotumika katika uundaji wa toponemia katika jamii. Lengo mahsusi la utafiti huu lilikuwa kupambanua miundo ya toponemia katika eneo la Mwimbi na Muthambi jimboni dogo la Maara. Maeneo haya yaliteuliwa kwa vile yalihusiana kilugha na kiutamaduni hasa katika suala la onomastiki. Nadharia ya Ujinaishaji ndiyo ilitumiwa kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kupitia kwa ya mahojiano ya ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala, na hivyo wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20 wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee iliweza kupatikana kwa urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya Kimwimbi na Muthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha michakato mbalimbali ya uundaji wa toponemia katika jamii.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.titleUpambanuzi wa Miundo ya Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenyaen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record