dc.description.abstract | Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu
unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia
hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke
vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na
kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka
wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia
ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia
pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani
katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika
leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko
yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji,
uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri
maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu
za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika
kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha
kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na
mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana
kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.. | en_US |